KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, October 26, 2010

Uchina na Marekani wajadili uchumi wao



Waziri wa fedha wa Marekani Geithner

Waziri wa Fedha wa Marekani, Timothy Geithner, amekutana na Makamo wa Waziri Mkuu wa Uchina, Wang Qishan, nchini Uchina, akiwa njiani kutoka mkutano wa mawaziri wa fedha wa nchi za G20, uliofanywa Korea Kusini.

Mawaziri hao ndio wanaoushughulika na uchumi katika nchi zao, na wanakutana mara kwa mara.

Wanasiasa hao ndio wamepewa jukumu la kupunguza mvutano kuhusu biashara baina ya Marekani na Uchina. Taarifa ya ubalozi wa Marekani mjini Beijing ilisema maafisa hao wawili, walijadili piya matayarisho ya mkutano wa viongozi wa mataifa ya G20, utaofanywa Korea ya Kusini, mwezi ujao.

Wanasiasa nchini Marekani, wamekuwa waki-ishinikiza serikali ya Rais Obama, kuwa i-ichagize Uchina iruhusu sarafu yake ya yuan, iachiwe kupanda kulingana na soko. Katika mkutano wa mawaziri wa fedha wa G20, uliofanywa mwisho wa juma hili, wakuu walikubali kuacha kushindana kushusha thamani ya sarafu zao, na kwamba IMF itasimamia makubaliano hayo.

Wadadisi wanaona, makubaliano hayo yamezimua mabishano, katika kile kinachoitwa, vita vya sarafu.


Wadadisi wanasema makubaliano hayana uzito, kwa vile hayakupewa muda maalumu kutekelezwa.
Lakini gavana wa benki kuu ya Uchina, amekiri kuwa nchi yake inahitaji kupandisha thamani ya yuan, lakini ifanye hivo taratibu.

No comments:

Post a Comment