KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Friday, October 22, 2010

Nusura aue mwanae kwa kumkuta na ganda la kondom


MWANAMKE mmoja [49] mkazi wa Mabibo jijini Dar es Salaam, jana nusura aue mtoto wa kumzaa mwenyewe kwa kumkuta na ganda la mpira wa kiume “ Kondom” kwenye mfuko wa madaftari wakati alipokuwa akikagua madaftari yake.
Mwanamke huyo alimuamuru mwanae huyo wa kiume asomae kidato cha pili amletee madaftari yake ili aweze kukagua alichokisoma kwa kipindi cha wiki nzima na kukutana na dhahama hiyo ambayo hakuitarajia machoni mwake .

Ilidaiwa kuwa, mwanamke huyo mfanyakazi wa Tanesco alichukua daftari hizo na kuingia nazo chumbani kwake na kuanza ukaguzi juu ya madaftari hayo na ilidaiwa wakati akiwa mwishoni wa ukaguzi huo aliona ganda hilo lililoanguka kutokea kwenye mifuko ya pembezoni mwa mfuko yalimokuwa madaftari hayo.

Ilidaiwa hakuamini macho yake kwanza kwa kuwa aina hiyo ya mpira hakuwahi kuiona wala kuisikia na alimuita mdogo wake mmoja wa kike aliyekuja kumtembelea hapo wiki moja nyuma alimuonbyesha ganda hilo na kumuuliza ni la nini na alimbainishia kuwa ni ganda la kondom na mama huyo ilidaiwa jasho jembamba lilianza kumchuruzika na kuanza kulia akiwa chumbani kwake.

Ndipo alipomaliza kulia na kuona amepata nafuu alimuamuru mdogo wake huyo amuite mwanae huyo na alipoingia humo hakutaka kumuuliza swali lolote na alianza kwa kumpa kichapo bila mtoto huyo kutambua alikuwa na kosa gani.

Ilidaiwa kuwa, mdogo wake pamoja na msichana wa kazi waliingia chumbani humo kumuamuru aache kumchapa lakini juhudi zao hazikuzaa matunda na mtoto huyo kupiga kelele kutokana kipigo hicho, ndipo walipoamua wafungue geti kuomba msaada kwa jirani yao wa karibu ili akamwambie aache kumuadhibu kijana huyo.

Juhudi hizo ndizo zilizaa matunda na kwa heshima ya jirani yake huyo ndio mama huyo alikubali kumuaacha kumpiga mtoto huyo kwa kutumia mkanda wa suruali na fimbo ya fagio wa wima wa kufagilia ndani.

Hata hivyo ilidaiwa baada ya kumaliza kipigo hicho mtotto huyo alikuwa amechoka sana kwa kipigo hicho na aliweza kumjeruhi kidogo, mwanamke huyo aliwasha gari na kumkimbiza mwanae huyo hospitalini kwa matibabu.

Hata hivyo nifahamishe ilibahatika kuonana na mwanamke huyo siku iliyofuata na hakuwa tayari kuongelea suala hilo ka kuhofia kunukuliwa huku akiomba asirushwe kwenye mtandao huu.

“Ujue nilikuwa na hasira sana, umri huu, nimemkuta na ………., yesu wangu, Mungu anisamehe, inamana ameshaanza……, nitamuombea, ujue ukishamuacha mtoto hivyo atajua ni kawaida, mimi sikumuuliza lolote, mimi nimejua tu alitumia yeye

No comments:

Post a Comment