KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, October 22, 2010

Mapigano yasababisha maafa makubwa



Mauaji katika mpaka wa Kenya na Somalia

Takriban watu kumi na wawili wameuawa baada ya kuzuka kwa makabiliano makali kati ya wapiganaji wa kiislamu na makundi ya wapiganaji yanayounga mkono serikali, kwenye mpaka wa Kenya na Somalia.

Taarifa zinaelezea kuwa maiti nyingi zilitapakaa mitaa ya mji wa Mandera mpakani.

Shirika la umoja wa mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) limesema zaidi ya watu elfu tatu wamekimbilia nchini Kenya kufuatia mapigano hayo.


Kulingana na mwandishi wa BBC kundi la wapiganaji la Al Shabab lilitaka kuuteka tena mji wa Beled Hawo kutoka kwa makundi ya wapiganaji wanaounga mkono serikali lakini halikufanikiwa.

No comments:

Post a Comment