Mshindi wa mbio za medali ya dhahabu baada ya kushinda mbio za mita 100 Damola Osayemi ameonekana kutumia dawa ya kuongeza nguvu mwilini.
Rais wa shirikisho la michezo ya Jumuia ya Madola Mike Fennel amewaambia wandishi wa habari Delhi kuwa Osayemi ameomba afanyiwe majaribio mengine ili kuthibitisha matokeo ya awali.
Ombi lake limekubalika na matokeo yake ni baada ya kikao kitakachosikiliza kesi hiyo
Damola Osayemi
Osayemi, mwenye umri wa miaka 24 kutoka Nigeria alitangazwa kuwa bingwa baada ya bodi inayotawala mashindano kumnyang'anya Sally Pearson wa Australia ushindi katika hali ya utata.
Sababu zilizotolewa na bodi hiyo ni kwamba Sally alianza kukimbia kabla ya mlio wa bastola kulia.
Hii ni mara ya kwanza kwa mwanariadha kupatikana kutumia dawa za kuongezea nguvu mwilini kwenye mashindano haya mjini Delhi.
Osayemi alionekana kuwa na chembe chembe za dawa iliyopigwa marufuku ijulikanayo kama methylhexaneamine, ambayo ni hivi karibuni tu ambapo shirika la kupambana na utumiaji wa dawa za kuongezea nguvu mwilini kuipiga marufuku kwenye orodha yake.
Endapo vipimo vya pili vitathibitisha kuwa Osayemi alitumia dawa ya kuongezea nguvu basi Katherine Endacott, aliyemaliza wa nne nyuma ya Pearson na Osayemi atapandishwsa na kupokea medali ya fedha.
Hadi sasa hakuna maamuzi yaliyofikiwa kuhusu hatma ya medali, hadi jopo la wataalamu wa afya wathibitishe au wakose dawa za kuongzea nguvu katika vipimo vinavyofanywa kwa Osayemi
No comments:
Post a Comment