KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Saturday, October 9, 2010

Matokeo yatatoka mapema -NEC



TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetoa ahadi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu ndani ya siku tatu mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo.


Ahadi hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa NEC, Bw. Rajabu Kiravu, wakati alipokuwa akizungumza na wasimamizi wa uchaguzi huo.

Alisema tume hiyo im ejiandaa kwa kutoa matokeo hayo mapema iwezekanavyo na wataanza kwa kutangaza matokeo ya urais Novemba 3, mwaka huu.

Alisema mara baada ya kutangaza matokeo hayo yatafuatiwa kwa kutangazwa matokeo ya ubunge yakifuatiwa na yale ya udiwani.

“Tumejiandaa vya kutosha na hatuna sababu za kuchelewesha matokeo kwa kuwa maandalizi yote ya yanayohusiana na uchaguzi yamekamilika, zikiwemo karatasi za kura, wino, usafirishaji wa vifaa vya kupigiakura” Kiravu.

Pia alsiema katika maandalizi hayo tume hiyo imepanga kukutana na vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi ambapo imepanga Oktoba 18 hadi 22 kukutana na wagombea kwa upande wa Tanzania Bara na Oktoba 27 kwa upande wa Visiwani Zanzibar

No comments:

Post a Comment