KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 20, 2010

Guinea yatakiwa kutangaza tarehe ya uchaguzi



Mkuu wa tume ya uchaguzi General Sangare


Kumekuwa na wito wa kimataifa kwa serikali ya Guinea kutangaza tarehe mpya ya duru ya pili ya uchaguzi wa urais kwa haraka iwezekanavyo.

Awali uchaguzi huo ulikuwa ufanyike siku ya Jumapili, lakini ukaahirishwa bila kutajwa tarehe ambapo utafanyika.

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa katika Afrika Magharibi, Said Djinnit, aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa kuahirishwa kwa uchaguzi kwa muda mrefu kunaweza kukasababisha machafuko.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani, (Philip Crowley) alisema uchaguzi huo ni muhimu kwa mustakbala wa Guinea.

Kuahirishwa kwa uchaguzi huo kunatokea wakati ghasia zikizidi kupamba moto Guinea, pamoja na mzozo juu uongozi wa tume ya uchaguzi.

No comments:

Post a Comment