KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 20, 2010

AU yaikosoa UN kwa kutosaidia wanajeshi wake




Askari wa AU

Viongozi wa Kiafrika wamelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuunga mkono kikamilifu wanajeshi wa Muungano wa Afrika wakati Umoja wa Mataifa ukitegemea wanajeshi hao kwa operesheni za kulinda amani.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria, Henry Odein Ajumogobia, alisema maombi ya kutaka wanajeshi wa Muungano wa Afrika kwenda kuhudumu sehemu nyingi duniani kama walinda amani yanazidi uwezo wake, na hivyo kusababisha operesheni hizo kukwama na machafuko kuongezeka.

Repoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ilikiri ukuaji wa kutegemea wanajeshi wa Afrika.

Bw Ban amesema opesheni za kulinda amani za Muungano wa Afrika zinapaswa kupokea uungaji mkono, na ufadhili sawa kama askari wengine wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment