KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, October 6, 2010

FIFA yaisimamisha Nigeria



Shirikisho la soka duniani FIFA limeisimamisha kwa muda Nigeria kushiriki katika mashindano ya kimataifa kutokana na serikali kuingilia kati mchezo huo.

Uamuzi huo ulitolewa Jumatatu baada ya wajumbe kadhaa wa shirikisho la soka la Nigeria (NFF) kufikishwa mahakamani.

Sheria za FIFA zinakataza serikali kuingilia kati wanachama wake.

"Kamati ya dharura ya FIFA imeamua leo....kusimamisha NFF mara moja kutokana na serikali kuingilia kati," FIFA ilisema.

"Wakati wa kusimamishwa kwa muda, NFF haitawakilishwa kwenye mashindano ya kanda, bara Afrika au kimataifa, pamoja na mechi za kirafiki," taarifa hiyo ya FIFA ilisema.

Kufuatia kupigwa marufuku huko kwa Nigeria kutocheza mechi za kimataifa, sasa hatma ya mechi ya mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Guinea mjini Conakry haijulikani

No comments:

Post a Comment