KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, September 13, 2010

Watu 3 wauawa Gaza
GAZA

Duru za maafisa wa afya wa Palestina zinasema watu watatu wameuawa na wengine wawili kujeruhiwa wakati wa shambulio la jeshi la Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza hapo jana. Jeshi la Israel limethibitisha kufanya shambulio la kombora lililonuiwa kuzuia jaribio la wanamgambo wa Kipalestina kuwashambulia wanajeshi wa Israel kwa roketi.

Mapema leo wanamgambo wa Kipalestina wamevurumisha roketi nchini Israel, ambalo jeshi la Israel linasema limeangukia kwenye uwanja ambao hakuwa na watu karibu na mji wa Sderot, karibu na mpaka na Gaza. Hakuna aliyejeruhiwa katika shambulio hilo. Takriban mashambulio saba ya maroketi au makombora yamefanywa dhidi ya Israel wiki iliyopita na Israel imejibu mashambulio hayo

No comments:

Post a Comment