KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 20, 2010

Watano mbaroni kwa ugaidi dhidi ya Papa



Polisi mjini London wanawashikilia watu watano kuhusiana na taarifa za uwezekano wa kuwepo tishio la kigaidi dhidi ya Papa Benedict.

Watu hao walikamatwa mjini London mwishoni mwa wiki baada ya maafisa wa kupambana na ugaidi kupokea taarifa za kijasusi kuhusu kuwepo kwa tishio hilo.

Watu hao wamepelekwa katika kituo kikuu cha polisi mjini London.

Maafisa wanaendelea na uchunguzi wao katika maeneo ambayo yanashukiwa kufanyika uvamizi unaohusiana na tishio hilo.

Katika taarifa iliyotolewa na Kikosi cha Scotland Yard, Polisi wanasema watano hao wamekamatwa katika msako uliofanywa na maafisa katika kamandi ya kupambana na ugaidi.

Wanashikiliwa kwa tuhuma za kupanga, kuandaa au kushawishi vitendo vya ugaidi chini ya sheria ya ugaidi ya mwaka 2000.

Umri wao ni miaka 26, 27, 36, 40 na 50. Walikamatwa katika maeneo ya biashara ambako msako ulikuwa ukifanyika.

Maeneo ya makazi kaskazini na mashariki mwa London pia yanafanyiwa msako.

No comments:

Post a Comment