KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 14, 2010

Walimu 14 mbaroni kwa wizi wa mitihani, Songea, Mwanza




WALIMU wakiwemo na wasimamizi 14 wa shule za msingi katika manispaa ya Mwanza na Ruvuma, wanashikiliwa na polisi kwa tuhuma za wizi, na kuwafanyia mitihani wanafunzi katika mitihani wa taifa ya darasa la saba iliyomalizika juzi.
Watuhumiwa hao tisa wamepatikana mkoani Ruvuma na watano mkoani MWanza.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Michael Kamhanda, alisema katika mtukio hayo pia wamo walimu wakuu wawili wa shule ya msingi ya Ruvuma na Kipera, wanatuhumiwa kusambaza majibu ya mitihani kwa kutumia ujumbe mfupi wa maneno kwa simu ya mkononi.

Mkoani Ruvuma wasimamizi waliopatikana na kosa hilo ni Daniel Mbise (59), Imelda Njogopa (39) na Doris Ngongi, Zainab Kantinga (44), Lucy Chiuko (36), Evalista Luambano (36) na Renata Benedicta (29).

Na mwalimu mkuu wa Kipera ni Cresensia Komba shule ya Ruvuma ni mwalimu Cesilia Ndomba.
Kamanda Kamhanda alisema, walimu hao wote wka pamoja walishirikiana kuiba mitihani hiyo na ksuambaza majibu wa watahiniwa hao.

Kamanda huyo alisema, walimu hao walikuwa wakisambaza majibu hayo ya masomo ya hisbati na kiswahili kwa njia ya ujumbe mfupi wa simu huku wengine walikuwa wamekaa maeneo ya vyoo vya shule.

Huko mkaoni MWanza nako walimu watano wamekamatwa baada ya kukutwa wamejifungia kwenye nyumba wakifanya mtihani wa somo la kiingereza na kujitayarisha kutoa majibu hayo kwa watahiniwa.

Kamanda wa Polisi MWanza, Simon Sirro, alithibitisha tukio hilo na kusema kuwa tukio hilo limetokea huko Sengerema walimu hao walikutwa wamejifungia chumbani wakijibu mtihani huo wa Kiingereza baada ya kulipwa Shilingi 1,329,500.

Sirro alisema,walimu hao ni wa Shule ya Msingi Nyamzumla iliyopo wilayani humo, na walikutwa majira ya saa 5 asubuhi, juzi, wakiwa wamejifungia nyumbani kwa mkuu wa shule hiyo wakijibu mtihani huo.

Kamanda Sirro alidai, walimu hao walikamatwa baada ya msamaria mwema kutoa taarifa kituo cha polisi na polisi walipiowasili eneo hilo waliwakuta walimu hao wakifanya mtihani huo wakiwa wamejifungia ndani humo wakiwa na karatasi nyembamba 50 za majibu ya mtihani huo

Walimu hao watafikishwa mahakani mara baada ya kukamilika upelelezi

No comments:

Post a Comment