KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, September 23, 2010

WAGOMBEA wa urais wa Zanzibar, jana wameushangaza umma baada ya kutoionekana katika mdahalo maalum!WAGOMBEA wa urais wa Zanzibar, jana wameushangaza umma baada ya kutoionekana katika mdahalo maalum uliowataka kuwakutanisha wagombea hao kushiriki mdahalo ulioandaliwa na asasi za kiraia.
Wagombea hao wapatao sita jana wameukacha mdahalo na kuhudhuriwa na mgombea mmoja wa Chama Cha Wananchi [ CU, Seif Sharrif Hamad na wenzake kutohuduria mdahalo huo.

Mdahalo huo uliofanyika jana, katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View na kuhudhuriwa na taasisi mbalimbali za kiraia kwa lengo la kutoa fursa ya wagombea kuulizwa maswali na wananchi moja kwa moja.

Waliogoma kuhudruria mdahalo huo ni pamoja na mgombea kutoka vyama vya CCM, NCCR - Mageuzi, Tadea, NRA, AFP na Jahazi Asilia .

UIkiacha kutoshiriki kwa mgombea wa CCM, DK. Shein kutohudhuria kwa kuwa walizuiliwa na KAtibu Mkuu wa chama hicho Yusuph Makamba wengine imedaia kuwa hawakushiriki kwa kukosa posho iliyowataka kuhudhuria mdahalo huo.

Hata hivyo Katika mdahalo huo, Maalim Seif alisema akipewa ridhaa kuongoza ataunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa akipata ridhaa za wananchi, pia atazijengea uwezo taasisi za kiraia ili ziweze kujitegemea pamoja kuwapatia wataalamu

No comments:

Post a Comment