KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, September 23, 2010
Mgodi waporomoka Burundi
Barundi
Takriban watu 10 wamefariki dunia baada ya mgodi wa dhahabu kuporomoka nchini Burundi, kilomita 120 kaskazini mwa mji mkuu.
Watu wengine watatu waliojeruhiwa katika ajali hiyo wamepelekwa hospitali.
Mamlaka ya jimbo la Kayanza, ambapo ajali hiyo imetokea, ameiambia BBC kuwa watu hao walikuwa wakichimba madini kinyume cha sheria.
Mwandishi wa BBC alisema licha ya Burundi kuwa na utajiri wa madini, kuna migodi michache iliyo rasmi na hata hiyo hutumia
vifaa duni na usalama ni mdogo.
Migodi mingi midogo iliyopo magharibi na kaskazini mwa Burundi hutumiwa na wanakijiji wanaotumia majembe ya kusukuma kwa mkono na plau.
Burundi ni miongoni mwa nchi maskini duniani na imetoka kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka 12 iliyotikisa uchumi wa nchi hiyo.
Madini ya kutengenezea simu
Mwandishi wa BBC Prime Ndikumagenge aliyopo kwenye mji mkuu, Bujumbura, alisema ajali za kwenye migodi katika kipindi hichi cha mwaka, hutokea mara kwa mara wakati mvua za awali zinapoanza.
Migodi kaskazini mwa mji wa Kayanza pia ina utajiri wa madini, yanayotumika kutengenezea simu za mkononi.
Victor Ntakirutimana, afisa tawala wa wilaya ya Kabarore huko Kayanza ambapo tukio hilo lilipotokea, ameiambia BBC wanakijiji wengi hawaoni tabu kujitia hatarini kupata angalau kiwango kidogo cha madini kwani ina thamani kubwa.
Raia pia husema ni imani ya wachimba migodi kuwa watu wengi wakifariki dunia ndani ya mgodi ni ishara kuwa mgodi huo una utajiri mkubwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment