KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, September 16, 2010

UN:Lazima Sudan ifanikishe Kura ya maoni


Sudan kujiandaa Kura ya maoni


Baraza la usalama la Umoja wa mataifa limetoa wito kwa pande zote mbili nchini Sudan kuchukua hatua za dharura kuhakikisha kuwa kura ya maoni inayopangwa kufanywa Januari mwakani inafanyika.

Raia wa Sudan Kusini wanapiga kura kuamua iwapo wajitenge na serikali ya Khartoum na Jimbo la Abyei linapiga kura kuamua litajiunga na upande upi iwapo Sudan kusini itajitenga na kaskazini.

Kura hizo ni miongoni mwa mabadiliko yaliyoafikiwa katika mkataba wa amani wa mwaka wa 2005 uliomaliza vita vya zaidi ya miongo miwili nchini humo. Hata hivyo kumekuwa na shutuma nyingi za kucheleweshwa kwa shughuli hiyo.

Rais barack Obama anahudhuria mkutano unaojadili mstakabali wa Sudan wakati wa mkutano mkuu wa Umoja wa mataifa mjini New york

No comments:

Post a Comment