KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

UN yasema wasichana wadogo walibakwa DRC



Umoja wa Mataifa umesema takriban vijana wadogo wapatao thelathini walikuwa miongoni mwa waathiriwa wa ubakaji mkubwa uliotokea mashariki kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa ilisema vijana hao walikuwa na umri kati ya miaka kumi na mbili hadi kumi na saba.

Umoja wa Mataifa umekosolewa kwa kushindwa kuzuwia shambulizi hilo la ubakaji lililotokea kilometer thelathini tu kutoka vituo vyao vya askari wa kulinda amani.

Sasa Umoja wa Mataifa unaamini kuwa watu wasiopungua mia mbili na arobaini walibakwa katika uvamizi uliofanywa na waasi wa Congo na wale wa Rwanda katika jimbo la Kivu ya Kaskazini kati ya mwisho wa July na mapema mwezi August.

Wafanyakazi wanaotoa misaada na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa walifahamu waasi walikuwa kwenye mji wa Luvungi na vijiji vilivyo karibu mashariki mwa Congo siku moja baada ya mashambulio yalivyoanza Julai 30, shirika la kutoa misaada ya matibabu la International Medical Corps (IMC) lilisema.

No comments:

Post a Comment