KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Hatua ya Ufaransa kuwafukuza jamii ya Roma yapingwaMaandamano dhidi ya sera ya serikali ya Ufaransa ya kuwafurusha watu wa jamii ya Roma yanafanyika kote nchini baadaye hii leo.

Makundi ya kupinga ubaguzi wa rangi na mengine yanayopinga sera hiyo, ambayo yalishuhudia karibu watu elfu moja wa jamii ya Roma wakirejeshwa Romania na Bulgaria mwezi uliopita, yanatarajia kuwa zaidi ya watu elfu thelathini wataandamana mjini Paris pekee.

Kumekuwa na shutma kali kutoka kwa jamii ya kimataifa juu ya hatua ya kuwafukuza watu hao, pamoja na masuali kuhusu uhalali wao wakuishi Ufaransa.

Vaticani na Umoja wa Mataifa ni miongoni mwa taasisi zinazopinga uamuzi huo, wakati Rais Sarkozy akikabiliwa na uasi ndani ya serikali yake.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Francois Fillon, alisema kuwa hakupendezwa na hatua ya kuhusisha wageni na uhalifu. Naye waziri wa mambo ya nje Bernard Kouchner alisema anafikiri kujiuzulu, huku waziri wa ulinzi , Herve Morin, akihoji sera ya usalama wa taifa.

Mawaziri wa mambo ya ndani wa Muungano wa Ulaya wanakutana siku ya Jumatatu kujadili suala hilo.

Lakini kura za maoni zinaonyesha kuwa zaidi ya nusu ya raia wa Ufaransa wanahisi serikali inafuata sera sahihi

No comments:

Post a Comment