KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Nigeria yahofia mashambulio



Jeshi la Nigeria linaendesha msako wa pamoja na polisi kusini mwa mji wa Maiduguri baada ya wimbi la mauaji yanayosadikiwa kufanywa na kundi la kiislam la Boko Haram.

Polisi wamepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki usiku baada ya kurushiana risasi kulikofanywa na waendesha pikipiki.

Watu kumi na wawili wakiwemo polisi saba wamekufa mwezi uliopita.

Mapigano kati ya kundi la Boko Haram na polisi mwezi Julai 2009 yalisababisha mamia kufa.

Mapigano ya karibuni yalitokea Jumapili na kusababisha watu wawili kufa akiwemo afisa mmoja wa polisi.

Pikipiki zimezuiliwa kuendeshwa mjini kuanzia 1800 mpaka 0700.

'Huu ni mwanzo tu,' alisema kamishna wa polisi wa jimbo la Borno, Ibrahim Abdu.

'Kama mbinu hii haitafanikiwa tutapiga marufuku kabisa pikipiki zote jimboni hapa' alisema, linaarifu shirika la AFP.

Ghasia zilianza mwaka uliopita wakati Boko Haram waliposhambulia kituo cha polisi kilichopo Maiduguri kabla mapigano hayo kuenea maeneo ya jirani.

Wengi wa waliokufa walikuwa watu wanaounga mkono kundi hilo ambalo pia kwa wenyeji linajulikana kama Taliban na linataka kuona sheria za kiislam zinatumika nchini Nigeria.

Kundi hili linapinga elimu ya kimagharibi na linashutumu serikali ya Nigeria kutawaliwa na mawazo ya kimagharibi.

Kiongozi wa kundi hilo Mohammed Yusuf ni miongoni mwa waliouawa, inasemekana baada ya kukabidhiwa kwa polisi akiwa hai

No comments:

Post a Comment