KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Mpango wa mabilioni ya dola kwa miundo mbinu Marekani



Rais Barrack Obama ameelezea mpango wake wa miaka sita wa kuwekeza dola billioni 50 nchini Marekani katika sekta za barabara, reli na katika njia za kukimbilia ndege.

Zaidi Obama ameahidi kuekeza dola billioni 50 nchini katika sekta za barabara, reli na katika njia za kukimbilia ndege.

Mpango huo ni moja wapo ya mipango ya kuichumi inayolenga kukuza ajira na kujaribu kuzuia chama chake cha Democratic kushindwa katika uchaguzi wa wabunge unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, baadaye mwaka huu.

Katika hotuba yake kwa watu wa jimbo la Milwaukee, Obama alisema kuwa atajenga maelfu ya kilomita za barabara kuu, reli na kukarabati mitambo ya usalama katika viwanja vya ndege na kwnye barabara.




Mpango huu wa Obama ni mojawapo ya nyenzo anazonuia kubuni nafasi za kazi na kujaribu kuzuia chama chake kupoteza ushswishi katika uchaguzi unatarajiwa wa Congress mwezi Novemba.

Wanasiasa wa chama cha Republican wamekosoa mpango huo na kusema hautanikiwa na kuwa utaongeza gharama za matumizi ya fedha za serikali

No comments:

Post a Comment