KARIBU MAISHANI
KARIBU MAISHANI
Thursday, September 2, 2010
Mafuriko makubwa yatokea Sudan kusini
Maafisa wa afya wamesema, takriban watu 57,000 wamelazimika kuhama makazi yao kutokana na mafuriko makubwa kusini magharibi mwa Sudan kwa kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
Mvua kubwa ilionyesha Aweil, mji mkuu wa jimbo la kaskazini la Bahr al-Ghazal, limesababisha eneo hilo kufunikwa na maji.
Mwandishi wa BBC alisema mafuriko hayo yanasababisha changamoto nyingine katika daftari la kujiandikishia wapiga kura ambalo tayari limechelewa.
Sudan kusini inatarajiwa kupiga kura ya kujitenga na upande wa kaskazini katika kura ya maoni ya mwezi Januari.
Changamoto
Mwandishi wa BBC Peter Martell huko Sudan kusini alisema mafuriko hayo yanaongeza huzuni kwenye eneo hilo lisilo na maendeleo ambalo bado linahangaika kujijenga upya baada ya vita na upande wa kaskazini vilivyodumu kwa miongo miwili.
Sudan
Waziri wa afya wa Sudan kusini Luka Monoja ameonya, "Mvua zitaendelea mpaka Oktoba, kwa hiyo hali inaweza kuzidi kuwa mbaya."
" Hali mbaya imeibuka Aweil- zaidi ya theluthi tatu ya mji huo umekumbwa na mafuriko na nyumba nyingi kuporomoka.
"Tumeshuhudia watu wote wamelazimika kukimbia nyumba zao, na sasa wanaishi barabarani, kwasababu barabara ni eneo pekee kwenye mji huo ambao uko kwa juu."
Mwandishi wetu alisema serikali ya kusini na mashirika ya kutoa misaada yamekuwa yakiwasaidia wale waliohama makazi yao, na changamoto ni kubwa sana.
Alisema, umoja wa mataifa umetoa msaada wa chakula kwa takriban nusu ya idadi ya watu wa kusini kwa mwaka huu pekee.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment