KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, September 6, 2010

Darasa la 7 waanza mitihani leo



WANAFUNZI wa darasa la saba kote nchini, leo wameanza kufanya mitihani yao ya kuhitimu eli mu ya msingi.


Wanafunzi hao leo wameanza mitihani kwa somo la Sayansi ambayo imemalizika hivi punde na wanasubiri kuingia kufanya mitihani wa hisabati ambayo wanafunzi waliowengi kuhofia mtihani huo.

NIFAHAMISHE ilibahatika kuwahoji wanafunzi wawili watatu ambao wametoka katika mtihani wa sayansi, walidai kuwa mtihani ulikuwa ni wastani na wengi wao kuwa na mawazo katika mtihani tarajio watakaoingia katika kipindi cha pili

Mwanafunzi huyu Athumani alisema “ Dada mtihani wa sayansi si mgumu sana, ni kawaida ila, ila hisabati sijui utakujaje?” alihofu mwanafunzi huyu


Mitihani hiyo inatarajia kumalizika kesho.

Katika kumaliza elimu hiyo ya msingi Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Imeruhusu wanafunzi wote wa kike waliopata ujauzito mashuleni kufanya mitihani hiyo.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Mahiza, aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jana.
Mahiza alisema, “elimu ya msingi ni ya lazima kwa kila mtoto nchini hivyo tunawaruhusu wanafunzi hao kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya msingi” .

“Kama tulivyofanya mwaka jana… mwaka huu tunafanya hivyo kwa sababu elimu ya msingi ni ya lazima kwa kila mtoto, wapo waliopata ujauzito kwa bahati mbaya, tunategemea miongoni mwao wapo watakaojiunga na vyuo,” alisema Mahiza.

Jumla ya wanafunzi 924,280 wanatarajia kuhitimu darasa la saba mwaka huu,ambapo wasichana ni 471,827 na wavulana ni 452,453.

No comments:

Post a Comment