KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Boti Zingine Mbili Zazama na Kuua Zaidi ya 200 Kongo



Zikiwa zimepita wiki chache baada ya boti ya abiria iliyojaza watu kupita uwezo wake kuzama na kuua watu 140 nchini Jamhuri ya Kongo, boti nyingine mbili zimezama nchini humo na inahofiwa watu zaidi ya 200 watakuwa wamepoteza maisha yao.
Huku somo la kujaza watu wengi kuliko uwezo wa boti likiwa halijawaingia watu akilini, watu zaidi ya 200 wanahofiwa kufariki baada ya boti zingine mbili kuzama kwenye mto katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

Mojawapo ya boti hizo mbili, ilikuwa ni boti ya mafuta na haikutakiwa kubeba abiria hata mmoja, ilishika moto kutokana na hitilafu kwenye injini yake wakati ikikatiza kwenye kijiji cha Mbendayi kwenye mto Kasai karibu na mpaka wa Angola.

Watu waliokuwa kwenye boti hiyo walijirusha kwenye maji ili kunusuru maisha yao na kupelekea wengi wao kupoteza maisha kwa kuzama.

Boti nyingine ilikuwa ni ya abiria, ilikuwa imebeba abiria takribani 300 ambao ni zaidi ya nusu ya uwezo wa boti hiyo, ilizama baada ya boti hiyo kugonga mwamba.

Wizara ya habari ya nchini humo imethibisha vifo vya watu 70 kutokana na ajali hiyo. Watu 15 waliokolewa.

No comments:

Post a Comment