KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Tuesday, September 7, 2010

Jeshi la Polisi laimarisha ulinzi KariakooJESHI LA POLISI Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limeimarisha ulinzi katika maeneo ya Kariakoo kutokana na eneo hilo kukabiliwa na wingi wa watu na wafanyabiashara kuendesha shughuli zao usiku na mchana.


Hayo yalisemwa jana na Kamanda Wa Jeshi hilo, Suleimani Kova wakati alipokuwa akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari ofisini kwake.

Kova amesema kuwa jeshi hilo limeamua kuimarisha ulinzi maeneo hayo kutokana na kuwa na ushirikiana wa wafanyabiasha kutoka nchi jirani za Kenya na Uganda kufanya biashara eneo hilo usiku na mchana.

Hivyo kutokana na sababu hizo jeshi hilo limeimarisha ulinzi na kumwaga askari maeneo hayo kutokana na eneo hilo kukabiliwa na wingi wa watu kutoka ndani ya nje ya nchi.

Kwa kipindi hiki kinachoelekea sikuuu ya Idd maeneo hayo yamekuwa na changamoto nyingi hasa za wizi na matapeli kutoka kona mbalimbali za jiji kujikita eneo hilo kuendesha shughuli zao hizo

No comments:

Post a Comment