KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 2, 2010

Wazanzibari wapiga kura ya ndio

Raia katika visiwa vya Zanzibar wamepiga kura ya ndiyo, itakayowezesha katiba kubadilishwa, ili kuruhusu kuundwa kwa serikali za muungano.

Kwenye kura ya maoni iliyofanyika Jumamosi, asilimia 66.4 ya wapiga kura wameunga mkono mabadiliko hayo.

Chama tawala - CCM na kile cha upinzani CUF, vimekuwa vikihimiza watu kuunga mkono mabadiliko hayo na kupiga kura ya ndiyo, baada ya uhusiano wa vyama hivyo viwili kuonekana kuimarika kwa awamu.

Tume ya uchaguzi imesema upigaji kura umekuwa salama.

Ghasia na umwagikaji damu zimekuwa zikitawala uchaguzi wa Zanzibar katika siku za nyuma.

Kisiwa cha Zanzibar, kina utawala wake wa ndani chini ya Jamhuri ya Tanzania.

Kufuatia matokeo hayo, sasa katiba itafanyiwa marekebisho kwa haraka kwa ajili ya uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi October mwaka huu.

Baraza la wawakilishi la Zanzibar linatarajiwa kukutana baada ya wiki moja ili kuidhinisha marekebisho hayo mapya ya katiba.

Matokeo ya kura hiyo yametangazwa rasmi na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi wa Zanzibar Khatib Mwinyachande.

No comments:

Post a Comment