KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 16, 2010

Vitendo hivi hadi lini jamani?


WAKATI wengine wakiiba watoto mahospitalini kwa kukosa uzazi na sababu zingine tofauti, wengine wanatupa watoto na kutafutwa na jeshi la polisi kwa vitendo hivyo.

Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam, linamsaka kwa udi na uvumba aliyetupa mtoto wa kike mwenye umri wa siku moja aliyekutwa ametupwa eneo la Vijibweni.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa mtoto huyo alikutwa juzi, amelazwa eneo hilo na mtu huyo kutoweka na kumuacha mtoto huyo mahalai hapo.

Amesema hadi kufikia jana, hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo na uchunguzi bado unaendele na mtoto huyo alichukuliwa na kwenda kuhifadhiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hali yake ya kiafya inaendela vizuri .

No comments:

Post a Comment