KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 16, 2010

Afa kwa upepo wa gari

JOHN Hussein (45) mkazi wa Kiwalani, amefariki dunia baada ya kuchanika mwili wakati alipokuwa akijaza upepo katika gari.


Kamanda wa Polisi wa Wilaya Ilala, Faustine Shilogile, alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa 8:00 mchana, huko Kiwalani kwenye gereji ya kampuni ya Mohamed Interprises.

Shilogile alisema kuwa, marehemu huyo alifariki baada ya kugawanyika vipande na kupealekea utumbowake kutoka nje kutokana na kupata ajali alipokuwa akijaza upepo kwenye gari.

Alisema, alikuwa akiziba pancha kwenye tairi ya gari aina ya Scania lenye Trailer mali ya kampuni hiyo.

Alisema madhara yalitokea baada ya gari hilo kwenda kugonga bomba la gari lingine lililokuwa limeegeshwa gereji humo na kusababisha kutoka upepo kwa nguvu na kumpoteza ma rehemu huyo.

Marehemu huyo aliweza kuchanika vipande viwili kuanzia miguuni hadi kitovuni na utumbo wake kutoka nje na hatimaye kufariki dunia papo hapo na maiti imehifadhiwa hospitali ya Amana.

No comments:

Post a Comment