KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 16, 2010

UN yahimiza misaada zaidi kwa Pakistan.

Wiki mbili baada ya mafuriko kuanza nchini Pakistan, bado kuna idadi kubwa ya watu ambao bado wanahamishwa kutoka maeneo yenye hatari.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon, amesihi dunia kuzidisha usaidizi wake kwa nchi ya Pakistan iliyoathirika vibaya kutokana na mafuriko hayo.

Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Pakistan na makamu wake, Ban amesema Pakistan imesimama bega kwa bega na dunia nzima katika operesheni za wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa na kwamba dunia nzima lazima isaidia nchi hiyo.

Ameelezea ziara yake nchini humo kuwa ni ya kuvunja moyo kwake na kwa ujumbe wake.

''Sitawahi kusahau uharibifu na mateso niliyoshuhudia hii leo. Nimetembelea maeneo mengi ambayo yamepitia majanga ya kiasili kote duniani, lakini hakuna kinachokaribia nilichoshuhudia'', bw. Ban amesema baada ya kuzuru maeneo yaliyoathirika vibaya.

Amesema kuwa kiwango cha janga hilo ni kubwa mno, na watu wengi, katika maeneo mengi wanahitaji msaada.

Shirika la Umoja la Mataifa limetoa ombi la dharura la dola nusu billioni kwa nchi ya Pakistan.

Takriban mtu mmoja kati ya kumi ameathirika moja kwa njia moja au nyingine. Huenda , watu millioni ishirini, ambayo ni humusi ya watu nchini Pakistan wameathiriwa na mafuriko hayo.

Zaidi ya watu 1500 wamefariki dunia kufuatia mafuriko hayo.

No comments:

Post a Comment