KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 2, 2010

Tume ya kimataifa kuichunguza Israil

Ripoti kutoka Israil, zinasema serikali imekubali kushirikiana maafisa wa umoja wa mataifa, katika uchunguzi wa shambulio lililofanywa na maafisa wake dhidi ya meli ya misaada iliyokuwa ikielekea Gaza.

Shambulio hilo la mwezi Mai lilisababisha mauaji ya raia tisa wa Uturuki.

Baraza la mawaziri la Israil, limeripotiwa kukubali matokeo ya uchunguzi uliofanywa na tume za Israil kutumika na maafisa wa umoja wa mataifa katika uchunguzi wao.

Tume hiyo ya kimataifa iliyotangazwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, inajumuisha mwakilishi mmoja kutoka Uturuki.

Awali Israil, ilisema hakuna haja ya uchunguzi wa kimataifa kuhusu tukio hilo.

Waangalizi wanasema hatua ya Israil kukubali kushirikiana na tume hiyo ya kimataifa iliyoundwa na Ban Ki Moon, inaonyesha kuwa imebadili nia yake.

Waziri Mkuu wa Israil Benjamin Netanyahu, amesema nchi hiyo haina lolote la kuficha na kwamba ni vyema uchunguzi wa wazi ukifanywa.

Tume hiyo ya kimataifa inatarajiwa kuancha kupokea ushahidi kuanzia wiki ijayo.

Israil imekuwa ikisusia kushiriki katika uchunguzi wa Umoja wa Mataifa katika maswala mengi na huenda sasa imeamua ingetaka sauti yake isikike.

No comments:

Post a Comment