KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 2, 2010

Mafuriko Pakistan, misaada yakwama

Maelfu ya watu , wameachwa bila makao katika maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko nchini Pakistan.

Mashirika ya misaada na wanajeshi wanajaribu kufikisha misaada katika maeneo hayo, huku zaidi ya watu elfu moja wakiripotiwa kufa maji katika mafuriko hayo ambayo yameelezewa kuwa mabaya zaidi, kuwahi kuikumba nchi hiyo kwa muda mrefu.

Mashirika ya misaada, yanasema mojawapo wa matatizo makubwa wanayoakabili ni uwezo wa kuwapatia msaada wale wanaouhitaji sana.

Mafuriko yalikua ya nguvu zakutosha kusomba barabara na madaraja mengi.
Sehemu za mashambani, nyumba nyingi ni za udongo na haziwezi kustahamili nguvu za mafuriko. Katika sehemu fulani vijiji vizima vimetoweka. Kwingineko familia zinalala juu ya mapaa ya nyumba, chakula ni haba halikadhalika maji ya kunywa-kwa kua visima vingi vimeharibika.

Tayari Baadhi ya wakaazi wa maeneo yaliyoathiriwa sana, wako katika hali ya wasiwasi. Wengi wao, katika nyanda za juu za Kaskazini Magharibi walilazimika kukimbia makaazi yao mwaka jana wakati wa mapigano makali kati ya vikosi vya serikali na waaasi.

Kuhama kwao kulisababisha ugumu katika kuangalia ardhi zao na kuvuna mazao.

No comments:

Post a Comment