KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, August 26, 2010

Taliban watishia usalama UN Pakistan


Umoja wa Mataifa unasema unachunguza hatua zake za usalama wa wafanyakazi wa mashirika ya misaada nchini Pakistan, kutokana na onyo jipya kutoka kwa kundi la Taliban wa Pakistan.

Shughuli za misaada zitakuwa hatarini kuvurugika endapo Taliban watahatarisha usalama.

Afisa wa Marekani amesema kuwa kundi hilo linapanga kuwashambulia wageni wanaowasilisha misaada kwa watu walioathiriwa na mafuriko. Mashambulio ya aina hiyo hayajafanyika tangu mafuriko yatokee.

Kwa kipindi cha mwezi mzima Pakistan imekumbwa na mafuriko yaliyotajwa kama janga kubwa kuwahi kumkabili binadamu katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa zaidi ya watu milioni 17 wameathiriwa na mafuriko, nyumba milioni moja nukta mbili zimeteketea zikiacha watu milioni 5 bila makazi.

Wakati wimbi la mafuriko likizidi kutiririka kutoka kaskazini, maji yamevuka kizuizi kimoja huko Kot Almo katika jimbo la Sindh, na kutishia maelfu ya watu katika wilaya ya Thatta ya kusini waliokimbia kutoka nyumba zao.

Takriban watu elfu 400,000 wameambiwa waondoke miji ya Sujawal, Mil Pur Batoro na Daro.
'Mpango wa shambulizi'

Afisa mmoja wa Marekani asiyetaka jina lake litajwe ameiambia BBC kuwa, kundi lijulikanalo kama Tehrik-e Taliban linasemekana kuwa na mipango ya kushambulia raia wa kigeni wanaoshiriki shughuli ya kugawa chakula kwa watu walioathiriwa na mafuriko haya ya Pakistan.

Afisa huyo ameongezea kuwa Marekani inaamini kuwa mawaziri wa serikali za majimbo na wilaya huenda wako wanakabiliwa na hatari, ingawa hakutoa maelezo zaidi.

Msemaji wa Shirika la Afya Duniani, ameieleza BBC kuwa shughuli za ugavi wa misaada katika Khyber-Pakhtunkhwa na Baluchistan zimekumbwa na wasiwasi wa uwezekano wa mashambulizi.

Ahmed Farah Shadoul amesema kuwa vitisho hivyo vina maana kwamba itabidi tupunguze shughuli nzima, ikiwa na maana kwamba hatutoweza kuwafikia waathiriwa walio mbali

No comments:

Post a Comment