KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, August 26, 2010

Kichaa cha Mpishi Baada ya Kufukuzwa Kazi


Mpishi wa mgahawa mmoja nchini Marekani alizua kizaazaa kilichowakimbiza wapishi wote jikoni baada ya kuambiwa kuwa hahitajiki tena kwenye mgahawa huo.
Mpishi huyo wa mgahawa mmoja uliopo Florida, Marekani alionyesha hasira zake za kufukuzwa kazi kwa kufanya uharibifu jikoni.

Mpishi huyo aliing'oa kompyuta iliyokuwa imebandikwa ukutani jikoni kabla ya kuanza kumwaga mwaga kila kilichokuwa mbele yake.

Huku akiwarushia matusi wapishi wenzake, mpishi huyo alivunja sahani na vikombe na kuwafanya wapishi wenzake walikimbie jiko baada ya kuwatishia na kitu chenye ncha kali.

Hatimaye kichaa cha mpishi huyo kilitulizwa na mteja mmoja wa mgahawa huo ambaye hakujulikana jina lake ambaye alimpiga mtama wa nguvu mpishi huyo na kupelekea agaregare kwenye sakafu.

No comments:

Post a Comment