KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, August 24, 2010

Mwanamke akabiliwa na tuhuma za kujaribu kuua

MWANAMKE mmoja [jina kapuni][37] mkazi wa Kigogo, anakabiliwa na tuhuma za kujaribu kumuua mumewe wake kwa kumuwekea madawa ya kienyeji kwenye vyakula ili aweze kurithi mali zake.
Imedaiwa kuwa mwanamke huyo anamuwekea madawa ya kienyeji mumewe kwenye vyakula ili aweze kummaliza kwa minajiri ya kutimiza malengo yake ya kurithi mali zake.

Imedaiwa kuwa mume huyo aliyetambulika kwa jina la Hussein [61]ni mstaafu wa serikalini alimuoa mwanamke huyo miaka minne iliyopita.

Imedaiwa kuwa mwanamke huyo alibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume na baadae mwanamke huyo alianza kubadilika.

Imedaiwa kuwa mwanaume huyo anasumbuliwa na maradhi ya presha, miguu kuuma na alikuwa na mali mbalimbali ikiwemo na kuendesha miradi yake ikiwemo na kuwa na vyombo vya usafiri [daladala]vinavyofanya kazi jijini Dar es salaam.

Hivyo imedaiwa kuwa mumewe huyo alikuwa akisumbuliwa na maradhi hayo na mwanamke huyo kwa kuwa alichoshwa na baba huyo alianza kutumia fursa hiyo ya kumletea dawa za hizo kwa lengo la kummaliza

Imedaiwa kuwa mwishoni mwa wiki iliyopita ndugu wa mwanaume huyo walifika nyumbani hapo kwa minajiri ya kumjulia hali na waliona madawa hayo ya asili akiandaliwa baba huyo na walipomuhoji alijieleza ni dawa za kumsaidia matatizo yake ya presha hali ambayo ndugu hao walipinga asipewe kwa kuwa zilikuwa hazimsaidi.

Hata hivyo baba huyo alidai kuwa alivyozidiwa na hali yake hiyo mke wake huyo kila kukicha huwa anampa madawa ambayo mengine hayafahamu na kukiri kuwa anazidiwa na maradhi hayo kuongezeka.

Hivyo ndugu hao walichachamaa na kumbana mwanamke huyo awaeleze madawa hayo alikuwa akiyatoa wapi

Mwanamke huyo alianza ugomvi kwa kudai kuwa anaingiliwa madaraka ndani ya nyumba yake na kuwataka ndugu hao wamuache amuhudumie mumewe bila kuingiliwa na mtu na zogo kubwa kuzuka hali iliyofanya majirani wasikie mazogo hayo.

Katika ugomvi huo rafiki mmoja wa mwanamke huyo ambaye ni jirani yake alishajua siri itakuwa imegundulika kwa kwua huwa wanaendaga wote kufata madwa hayo na kutoa siri hiyo kwa mwanawamke mwingine ambaye ni hasimu wa mwanamke huyo kwa kuwa walishawahi kukwaruzana.

Siri hiyo ilitolewa kwa ndugu hao naw alichukua uamuzi wa kumchukua ndugu yao huyo kwa ajili ya kwenda kusimamia afya yake na kuogopa kumuacha na mke wake huyo kutokana na siri hiyo iliyotolewa na jirani huyo

No comments:

Post a Comment