KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 18, 2010

Mgomo wa kitaifa Afrika Kusini




Wafanya kazi waandamana kudai nyongeza ya mishahara

Wafanya kazi waandamana kudai nyongeza ya mishahara


Maelfu ya wafanya kazi wa umma nchini Afrika Kusini ikiwemo waalimu, maafisa wa polisi na wahudumu wa afya wanatarajiwa kufanya mgomo Jumatano hii wakidai nyongeza ya mishahara.

Muungano wa wafanya kazi COSATU na vyama vingine vya wafanya kazi hususan chama cha Waalimu nchini humo, SATU, wanadai nyongeza ya asilimia nane nukta sita, baadala ya asilimia saba iliyoafikiwa na serikali.

Akitangaza hatua hii kiongozi mmoja wa muungano wa wafanya kazi amesema mgomo huu utaathiri utoaji wa huduma katika sekta zote za umma.

Wiki jana wafanya kazi hao walifanya maandamano ya siku moja mjini Pretoria na Cape Town na kuikabidhi serikali malalamiko yao.

No comments:

Post a Comment