KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Wednesday, August 18, 2010

Majeshi ya India yauawa Kongo

Waasi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamewaua wanajeshi watatu wa kutunza amani ambao ni raia wa India.

Jeshi hilo la India limesema idadi kubwa ya watu waliokuwa wameshikilia mapanga wakiwa wamevalia chane za mchikichi walifanya mashambulio katika kituo kilichofunguliwa na askari hao cha kusaidia raia.


Wapiganaji wa Mai Mai

Washambuliaji hao wanaaminiwa kuwa wapiganaji wa Mai Mai, wakilaumiwa kuhusika na ghasia zilizotikisa eneo hilo kwa miaka kadhaa.

Jeshi hilo la India limesema , lengo la shambulio hilo la usiku haliko wazi.
Shambulio la msituni

Kundi la raia watano wa Kongo walikwenda kwenye kituo hicho, kinachosimamiwa na majeshi ya Umoja wa Mataifa, lijulikanalo kama Monusco, mjini Kirumba.

Taarifa kutoka jeshi la India lilisema, "Waliomba msaada katika kituo hicho. Wakati wakiwazungumsha walinzi, kundi la takriban waasi 50 walivamia kituo hicho kwenye msitu huo."

Askari hao walifyatua risasi na kuwafukuza waasi hao, lakini hapo tayari askari watatu waliuawa na saba kujeruhiwa.

Takriban askari 4,000 kutoka India ni sehemu ya majeshi ya kutunza amani ya umoja wa mataifa.

Mashambulio ya waasi ya mara kwa mara huko Congo yamezua maswali ya uwezo wa jeshi hilo la umoja wa mataifa kuwalinda raia.

No comments:

Post a Comment