KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, August 16, 2010

Mchezaji Afukuzwa Kwa Kugoma Kufunga Mwezi wa Ramadhan

Mchezaji maarufu wa Iran, Ali Karimi ambaye hutajwa kama 'Maradona wa Asia' amefukuzwa na timu yake kwa kugoma kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani na kuendelea kula na kunywa kama kawaida.
Taarifa ya klabu yake iliyotolewa jana jumapili ilisema kuwa imelazimika kumfukuza Ali Karimi kwa kuwa mtovu wa nidhamu na kutofunga mwezi mtukufu wa ramadhan.


Klabu yake ya Steel Azin FC iliendelea kusema kuwa Karimi ambaye alikuwa mchezaji bora wa bara la Asia kwa mwaka 2004, aliwatukana viongozi wa shirikisho la soka la Iran na viongozi wa timu walipojaribu kumshauri kuhusiana na kufunga mwezi mtukufu wa ramadhan.

Karimi mwenye umri wa miaka 31, hujulikana zaidi nchini Iran kama 'Maradona wa Asia' na anashika nafasi ya pili kwa kuichezea timu ya taifa ya Iran mechi nyingi. Anashika nafasi ya tatu kwa kuifungia timu yake ya taifa magoli mengi.

Katika historia yake, Karimi aliwahi kulisakata kabumbu kwa miaka miwili kwenye ligi ya Ujerumani, Bundesliga ambapo aliichezea Bayern Munich na kuifungia magoli manne katika mechi 50 alizocheza.
Kufukuzwa kwa Karimi kumekuja ikiwa ni siku chache baada ya Karimi kumkosoa mkurugenzi wa timu yake, Mostafa Ajorlou.

Mwezi wa Ramadhan umeanza siku ya Alhamisi nchini Iran na kwa mujibu wa sheria za Iran, waislamu wote wanatakiwa kufunga na wale wasiofunga wakiwemo ambao si waislamu hutakiwa kujizuia kula na kunywa kwenye sehemu za wazi.

Wajawazito, wanawake walio kwenye hedhi, wazee, wagonjwa, watoto na wasafiri hawalazimiki kufunga.
MNA - LOS ANGELES, The American football club Los Angeles Galaxy is eager to sign up Iran’s Steel Azin midfielder Ali Karimi, according to the team’s Technical Manager Heshmat Mohajerani.
The Iranian international player’s contract expires at the end of the current season. Karimi is not willing to play in any other Iranian team except his former club Persepolis; however, he cannot play in that team either since he quarreled with the team’s current coach Ali Daei.
Karimi is expected to travel to the U.S. to negotiate with the Galaxy officials within the next two weeks.
“Ali (Karimi) has two offers from LA Galaxy and the UAE’s Al Ahli, but I think he would prefer to play in the American major league soccer,” Mohajerani said.
Karimi played in Bayern Munich from 2005 to 2007 before leaving the team for Qatar SC.
The 32-year-old will probably join the well-known British midfielder David Beckham in Galaxy.

No comments:

Post a Comment