KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 16, 2010

Hajasaidiwa kwa kuvaa nguo fupi


MSICHANA mmoja [27] ambaye hakupenda jina lake lichapishwe kwenye mtandao huu, ameilalamikia kampuni moja binafsi, kwa kushindwa kumsaidia kwa kuwa alivaa nguo vupi.
Msichana huyo aliyeonekana kulalamikia tendo hilo la kutosaidiwa na mmoja wa mabosi ofisini hapo kwa kuwa bosi huyo hakupendezewa na vazi hilo.

Alidai kuwa jana, majira ya saa 5 asubuhi alitinga kwenye ofisi hiyo kwa ajili ya kwenda kumalizia mipango yake ya kazi ambayo alikuwa akifatilia na kusaidiwa na kampuni hiyo.

Alidai siku hiyo hakumkuta mtawala ambaye mara kwa mara alikuwa akimsaidia mambo yake hayo, na jana alitakiwa aingie katika chumba kingine akutane na mmoja wa wakurugenzi wa ofisi hiyo.

Hivyo wakati alipofika na kukutana na katibu muhtasi wake, alimjuza kuwa kutokana na vazi lake hilo anahisi asingeweza kusaidiwa na mkurugenzi huyo kwa kuwa huwa anakemea mavazi hayo.

Msichana huyo aliona labda ni roho mbaya aliyokuwa nayo sekretari huyo na kumuamuru amruhusu aingie hivyo hivyo huenda atampokea.

“ Sikuamini bosi huyo alinitaka nitoke nje ya ofisi hiyo na kuniambia nina utovu wa nidhamu”

Hivyo kutokana na kitendo hicho cha kutosaidiwa kwa siku hiyo alikiiita ni cha binafsi na kumtuhumu bosi huyo alikuwa na ubaguzi wa kidini kwa kuwa hakuvaa vazi levu.

“Labda alitaka nivae hijabu na mimi sijazoea, nahisi anaubaguzi wa kidini kwa kuwa alinigundua mapema kwa kuwa huu ni mwezi wa Ramadhani.”alilalama

No comments:

Post a Comment