KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 9, 2010

Mafuriko yazidi kuleta hasara Pakistan

Mvua kubwa imeendelea kunyesha kaskazini magharibi mwa Pakistan, haswa katika maeneo ambayo maji yalikuwa yameanza kupungua katika siku za hivi karibuni.

Barabara zilizofunguliwa ilibidi zifungwe tena, huku ndege za helicopter zilizokuwa zinabeba msaada kwa watu millioni kumi na nne walioathirika kutokana na mafuriko zikishindwa kufanya kazi.

Maji yanateremka upande wa kusini kuelekea Mto Indus, na kulazimisha watu kuhamishwa kutoka eneo lenye utajiri wa kilimo katika jimbo la Sindh.

Jumuiya ya NATO ilisema itasaidia kuratibu usafirishaji wa misaada ya kimataifa katika mikoa iliyoathiriwa na mafuriko, kufuatia ombi la serikali ya Pakistan.

Mabwawa yahofiwa kupasuka

Maafisa nchini Pakistan wamesema mabwawa mawili katika eneo la Indus yako hatarini kupasuka kutokana na nguvu za mafuriko yanayoendelea kuteremka katika jimbo la Sindh kusini mwa nchi.

Wamesema saa 24 zijazo zitakuwa muhimu kwa usalama wa zaidi ya watu laki nne.

Hapo awali, watu laki mbili walihimizwa kuondoka kutoka nyumba zao, baada ya mabwawa mawili kupasuka.
Eneo kubwa la kilimo limegubikwa na maji.

Rais Zardai azomewa Uingereza

Rais Asif Ali Zardari, amekabiliwa na maandamano nchini Uingereza kuhusu uamuzi wake wa kuendelea na ziara badala ya kurudi nyumbani kushughulikia mafuriko yaliyoikumba Pakistan.

Waandamanaji waliokuwa wakimtaka arejee nyumbani walikusanyika mjini Birmingham, ambako Bw Zardari alitoa hotuba kwa mamia ya wanachama wa chama chake cha Pakistan People's Party.

Kuna wakati ambapo alizomewa na mzee mmoja ambaye alimrushia kiatu rais.

No comments:

Post a Comment