KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 20, 2010

DRC: Wapiganajii wabaka watu 170 katika siku nne
DRC: Zaidi ya watu mia moja wamebakwa katika wiki moja
Mashirika ya kutoa misaada na yale ya kibanadamu katika eneo la mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamedai kwamba makundi ya watu wenye silaha yamekuwa
yakiendeleza kampeini ya kuwabaka wanawake katika kipindi cha wiki chache zilizopita.
Msemaji wa shirika la kimataifa la kutoa misaada ya kimatibabu na kisaikolojia, International Medical Corps, Will Craigen amesema shirika lake limedhibitisha kuwa kumetokea visa mia moja na sabini vya dhuluma za kijinsia.

Visa hivi vimeripotiwa katika siku nne zilizopita katika vitongoji mwa mji wa Luvungi na vinadaiwa kutendwa na makundi ya wanamgambo.

Hili limebainika baada ya watu zaidi kujitokeza kutafuta msaada kutoka kwa mashirika hayo. Karibu watu mia mbili wamesema walibakwa katika kipindi cha siku nne tu

No comments:

Post a Comment