KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 20, 2010

Al-Megrahi: Je nini kilisababisha kuachiliwa kwake?


Ikiwa ni mwaka mmoja baada ya kuachiliwa mlipuaji wa ndege kwenye anga za Lockerbie huko Uskochi kwa misingi ya kibinadam, maseneta wanne wa Marekani wamerudia wito wao wa kuundwa kwa tume huru kuchunguza kuachiliwa kwa mtu huyo.

Wakati wa kuachiliwa kwake ilidaiwa kwamba Abdel Baset al-Megrahi anayeugua saratani alikuwa mgonjwa sana na alikuwa amesalia na miezi mitatu tu ya kuishi, lakini yu hai hadi leo.

Al-Megrahi aliyekuwa afisa wa ujasusi wa Libya ndiye mtu pekee aliyehukumiwa kwa ulipuaji wa ndege ya shirika la ndege la Pan Am iliyodunguliwa kwenye anga za Lockerbie, Uskochi na kuwauwa watu mia mbili na sabini mwaka 1988.

Wengi wa waathirika walikuwa raia wa Marekani.

Maseneta hao wa Marekani wanataka kupewa maelezo zaidi kuhusu ushauri wa kimatibabu uliowezesha kuachiliwa kwa Al- Megrahi.

Wametaka pia kupewa mawasiliano yaliyotokea kati ya serikali ya Uingereza na kampuni ya mafuta ya BP ya Uingereza ambayo ilihusika katika mashauriano na Libya wakati wa kuachiliwa kwa Al-Megrahi.

No comments:

Post a Comment