KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, August 23, 2010

CCM chaongeza idadi ya wabunge TanzaniaWakati k ampeni za u chaguzi mkuu nchini Tanzania zikiwa zimeanza rasmi c hama tawala nchini humo CCM kimezidi kuongeza idadi ya w abunge hata kabla ya uchaguzi wenyewe kufanyika.


Hayo yametokea baada ya mmoja wa waliokuwa wakiwania u bunge kupitia c hama cha u pinzani CHADEMA Bw Ezekiah Wenje wa jimbo la Nyamagan a m koani Mwanza k uenguliwa kuwania nafasi hiyo kwa madai kuwa si r aia wa Tanzania .

Hatua hiyo inamfanya Bwana Lawrence Masha ambaye alikuwa anawania nafasi hiyo kupitia CCM , akipambana na Bwana Wenje kupita bila kupingwa na hivyo kusubiri kuapishwa hata ya u chaguzi wenyewe unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba.Huku CCM w akichekelea ushindi bila kutoa jasho m gombea aliy eenguliwa Bw Wenje anaonekana kushangazwa na hatua hiyo , huku asisitiza kuwa yeye ni mzaliwa wa Tanzania.

Alisema baba, babu na wazazi wao wamezaliwa k atika w ilaya ya Shirati ambapo mama yake ndiye mzaliwa wa Kenya aliyeolewa Tanzania zaidi ya miaka 35 iliyopita .

Wafanyakazi wa sekta ya umma

Katika h atua nyingine c hama cha CCM kime sisitiza kuwa hakitaongeza mishahara ili kupata kura kutoka kwa w afanyakazi wa s ekta ya u mma ambao wanadai mishahara mikubwa.


Licha ya ku ra hizo za wafanyakazi hao kuwa muhimu, Rais Jakaya Kikwete amesema hatakuwa tayari kuahidi mishahara kwa kiwango ambacho serikali haina uwezo, na iwapo wafanyakazi watamuwekea masharti hayo basi kura hizo yuko tayari kuzikosa .


Naye m ratibu wa k ampeni z a CC M Bw Abdul- R ahman Kinana amesema h akuna mpango wa k upunguza safari za Rais Jakaya Kikwete licha ya k iongozi huyo kuishiwa nguvu jukwaani hivi karibuni m jini Dar es Salaam.


Hali hiyo imetafsiriwa kama uchovu kutokana na kazi nyingi , na hasa wakati huu ikiwa ni mwanzo wa kampeni ambapo atalazimika kuzunguka nchi nzima kuomba kura kwa Watanzania .


Bw Kinana amesema r atiba ya m gombea rais huyo inaen delea kama ilivyopangwa kwa kutumia magari na pia helikopta ili kuweza kuwafikia wananchi wengi zaidi katika kipindi hichi cha k ampeni .

No comments:

Post a Comment