KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Friday, August 6, 2010

Bakora 30 Kwa Wanaume Waliovaa Nguo za Kike

Kundi la wanaume 19 wa nchini Sudan ambao walivaa nguo za kike na kujipamba kama wanawake ili kuendeleza tabia yao ya ushoga wamecharazwa bakora 30 kila mmoja mbele ya mamia ya watu.
Wanaume 19 wa nchini Sudan ambao walivaa nguo za kike na kujipamba kwa vipodozi, walijikuta wakicharazwa bakora 30 kila mmoja mbele ya umati wa watu.

Mahakama ya nchini Sudan ilisema kwamba wanaume hao walivunja kanuni na sheria za maadili ya jamii.

Wanaume hao walitiwa mbaroni baada ya polisi kuwakuta kwenye sherehe moja nchini humo wakikata mauno kama wanawake.

Wanaume hao hawakupandishwa kizimbani na hawakuruhiwa kujitetea na mahakama ya mjini Omdurman ndiyo iliyopewa jukumu la kuamua shauri lao.

Muda mfupi baada ya mahakama kutoa hukumu hiyo, wanaume hao wakiwa bado wamevaa nguo za kike walijificha sura zao wakati wakicharazwa bakora 30 kila mmoja mbele ya mamia ya watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Wanaume hao pia walitakiwa kulipa faini ya paundi za Sudan, 1,000 (Takribani Tsh. laki tano).

"Ushoga si katika maadili yetu, haukuwepo hapa na anayetaka kuuingiza nchini atahukumiwa vikali sana", alisema afisa mmoja wa Sudan.

No comments:

Post a Comment