KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Sunday, July 11, 2010

Watu mia moja wauwawa Pakistan

Watu mia moja wameuwawa katika mashambulizi ya mabomu ya kujitoa mhanga katika kijiji kimoja nchini Pakistan kinachopakana na Afghanistan.
Manusura wa mlipuko
Manusura wa mlipuko

Watu wawili walishambulia kijiji cha Yakaghund katika mkoa wa Mohmand, na kuyaharibu majengo ya serikali, maduka na nyumba kadhaa.

Mohmand ni sehemu ya mikoa ya kikabila nchini Pakistan, ambako Taliban na al Qaeda wako na wanamgambo wengi.
Msemaji wa Taliban alisema kundi lao lilihusika na mashambulizi hayo.

Msemaji huyo, Ikramullah Mohmand alisema walikuwa wanalenga mkutano wa maafisa wa serikali na wazee wanaopinga Taliban kutoka kabila la Anbar Utmankhel.

Taarifa za hapo awali zilisema watu waliofariki dunia ni 50 na kusema mtu mmoja ndiye aliyefanya shambulizi hilo.

Hata hivyo, maafisa baadaye walisema kwa uchache watu 102 walifariki dunia na wengine zaidi ya 115 kujeruhiwa.

Miili mingine zaidi ilipatikana kutoka mabaki ya majengo na wengine walifariki hospitalini kutokana na majeraha.
Mlipuko huo ulitokea karibu na ofisi ya afisa wa serikali Rasool Khan, ambaye hakuumia.

Wazee wa kikabila walikuwa katika jengo hilo lakini hawakuumia, kulingana na mkuu wa utawala wa mkoa wa Mohmand Amjad Ali Khan.

Alisema shambulizi hilo lilionyesha "hali ya kukata tamaa" ya kundi la Taliban.


Mmoja ya milipuko hiyo iliharibu ukuta wa gereza na kusababisha baadhi ya wafungwa kutoroka, ingawa walioweza kutoroka hawakuwa wanagambo, alisema Rasool Khan.


Walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa miongoni mwa waliouwawa ni wanawake na watoto.Jimbo la Mohmand limekuwa uwanja wa mapambano makali kati ya jeshi la Pakistan na wanagambo wa Taliban.

No comments:

Post a Comment