KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Monday, July 19, 2010

Wanawake waomba namba ya simu ya mke aliyemkomesha mume


KUTOKANA na kuvutiwa na habari ya mwanamke kuua nguvu za kiume za mumewe asitoke nje ya ndoa, wanawake wengi wamekuwa wakimsumbua mwandishi wa habari hiyo atoe namba ya mwanamke huyo ili wawasiliane nae na wao wapate dawa hiyo wawafanyie waume zao
Wanawake wengi wamekuwa na hamu ama ya kumuona ama ya kutaka kupata mawasilino nae ili waweze kusaidiwa na dada huyo na wao waweke sawa hali za ndoa zao ambazo zinayumba kila kukicha kutokana na wanaume wao kutokuwa na uaminifu ndani ya ndoa zao.

“Tunaomba utupe namba ya huyo dada tusaidie, tunashida nae na sisi tunataka atupeleke kwa huyo mtaalamu wake, tumeshachoshwa na umalaya wa waume zetu” please

“ tunakuahidi kukupa zawadi pindi utakapotupa namba hiyo, hakika na mimi nikifanikiwa una zawadi nzuri” tumeshahangaika vya kutosha kwa wataalamu wa aina mbalimbali, lakini hawabadiliki, tumechoka, alidai dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Grace

Hadi habari hii inaandikwa mwandishi wa habari hii, ameshapata simu za wamama, wadada, zaidi ya kumi kutaka wapate maelekezo anapopatikana dada huyo.

No comments:

Post a Comment