KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 19, 2010

Amjeruhi baba wa kambo kwa kuchoshwa na kero zake


JOSEPHAT Maiko [16] mkazi wa Kigogo Mburahati, amemjeruhi baba yake wa kambo sehemu za usoni na kupelekea ashonwe nyuzi nane kwa kile alichodai ni kutokana na kuchoshwa na matendo anayomfanyia mama yake.
Kijana huyo machachari aliyechoshwa kuona kila uchwao mama yake mzazi akiteseka na tabia za baba huyo alichukua uamuzi huo ili kuweza kukomesha tabia ya baba yake.

Kijana huyo alichukua uamuzi huo juzi, baada ya mama yake akiwa katika ugomvi mkubwa ambao ulidaiwa haukuwa na kichwa wala miguuu kwa kile kilichodaiwa kuwa baba huyo alimtaka mama huyo ainuke usiku wa saa 7, ampikie supu wakati anatoka kwenye kinywaji.

Kutokana na kitendo hicho chakuchelewa kurudi nyumbani kwake na mama huyo kuonekana kuchoshwa na hali hiyo alimueleza mume wake huyo kwa muda huo alichoka na hataweza kumtayarishia supu hiyo kwa muda huo na kumuahidi angempikia asubuhi.

Jibu hilo hakupendezwa nalo na baba huyo alimsihi amtengenezee supu hiyo na mama huyo kuenndelea kugoma kupika kwa kuwa alichoshwa na ya kusumbuliwa usiku na mume wake huyo.

Hivyo kwa kuwa mama huyo alionekana kuendelea kugoma, ndipo kipigo cha haja kilianza kwa mama huyo na kuomba msadaa kwa mwanae huyo mkubwa aliyekuja kumtembelea mwishoni mwa wiki kumtaka aamke amsaidie.

Kijana huyo kwa kuwa alichoshwa na vitendo vya uonevu dhidi ya mama yake alishindwa uvumilivu na kuchukua uamuzi wa ghafla kuchukua chupa na kumtwanga nayo usoni na kumjeruhi baba huyo na kuchanika sehemu za usoni.

Mara baada ya tukio hilo baba huyo alikimibzwa zahanati ya karibu na alipatiwa matibabu na kushonwanyuzis nane katika mchano alioupata dhidi ya mwanae huyo.

Hata hivyo mama huyo alidai mume wake ni mkorofi kupita kiasi na hasa akilewa ukorofif unaongezeka na mara kwa mara huwa anapata vipigo kutoka kwa mume wake huyo kutokana na unywaji wa pombe

No comments:

Post a Comment