KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Wanane wauwawa katika mapigano Nigeria


Watu wasiopungua wanane wameuwawa katika shambulizi lililofanywa na watu waliojihami kwa mapanga karibu na mji wa Jos nchini Nigeria.
Mapigano ya Jos, Nigeria

Mapigano ya Jos, Nigeria

Kulingana na maafisa wa serikali, washambuliaji hao wasiojulikana walivamia kijiji kilichopo vioungani mwa mji wa Jos, na kuchoma nyumba kumi, mapema asubuhi ya Jumamosi.

Taarifa zinasema miongoni mwa waliouwawa ni familia ya kasisi mmoja katika kijiji hicho.

Mapigano kati ya Wahausa ambao ni Waislami na Wakristo wa kabila la Berom, yamesababisha vifo ya mamia ya watu mwaka huu.


Walishuhudia tukio hilo wanasema wanaume hao walishambulia familia ya Kasisi Nuhu Dawat katika kijiji cha Mazah, 12km kutoka mji mkuu wa jimbo hilo, Jos, na kuwauwa mkewe, watoto wawili na mjukuu wake.

Kasisi huyo alikimbia ili kunusuru maisha yake, na baadaye aliliambia shirika la habari la Reuters: " Yote namwachia Mungu aamue".

Mku wa jeshi la polisi katika jimbo la Plateau, Gregory Anyating aliliambia shirika la habari la Reuters kuwa serikali inajaribu kujua "chanzo cha ghasia hizo", na kuongeza kuwa mapambano hayakusambaa katika kijiji hicho.

Maandamano yaliyoambatana na ghasia katia miaka ya 2001, 2008 na 2010 yalisbabisha mamia ya watu kupoteza maisha yao.

Ingawa mapigano ni kati ya Waislamu na Wakristo, wachunguzi wa mambo wanasema sababu kubwa ni za kisiasa na kiuchumi

No comments:

Post a Comment