KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Sunday, July 18, 2010

Aliyemkomesha mume, ndoa yake iko matatani


MWANAMKE aliyetambulika kwa jina moja la Hasnat [33], ndoa yake iko mashakani baada ya familia ya mume kuchachamaa kwa kitendo alichomfanyia mume wake ili asitoke nje ya ndoa.
MWanamke huyo anatakiwa na familia ya mumewe kumuachia mumewe kwa kitendo alichokifanya kwa kuwa hamtendei haki na asipofanya hivyo kwa kipindi alichopewa basi ndoa yake itakuwa mashakani.

Chanzo cha habari hii, kutoka ndani ya familia hiyo kilidai kuwa, mwanamke huyo aliwekewa kiti moto na kutakiwa kuwa arudishe hali ya mumewe kwa kipindi kisichozidi mwezi mmoja kwa kuwa anamdhalilisha bila ya sababu za msingi.

Chanzo hicho kilidai kuwa mwanamke huyo hayuko tayari kurudisha hali ya mumewe huyo kwa kuwa alifanya hivyo ili mume wake apunguze tabia ya uzinifu aliyokuwa nayo.

Hivyo aliwambia ndugu hao kuwa wasiingilie mambo ya ndani ya ndoa yake na wawaachie wenyewe maswala hayo watamalizana wao wenyewe bila ya wao.

Kwa kuwa ndugu hao waliona kama ndugu yao anadhalilishwa kwa kitendo alichofanyiwa walimtaka mwanamke huyo aende alipofanya madawa hayo ili arudishe hali ya mumewe irudi kama awali na kumpa kipindi cha mwezi mmoja na kama hali hiyo isipotengemaa watamuamrisha ndugu yao amuache kwa kuwa alionekana kuwa ni anapenda ushirikina.

Bila kutarajia mwanamke huyo nae aliwajibu kuwa hayuko tayari kurudisha hali hiyo na anasubiri muda huyo ufike ili apewe talaka na endapo akiachana na mwanaume huyo ndipo atarudisha hali hiyo lakini akiendelea kuwa nae hatafanya hivyo.

“Kumbe ninyi mnaona raha ndugu yenu anavyonidhalisha kwa kutembea na wanawake wengine nje ya ndoa na habari kunifika mimi na hali hii imekuwa ikinisumbua toka nimeingia ndoa nay eye” na medhali nimeipata dawa yake mwisho wake wa kuzini umefika” alisema kwa kujiamini.


Juhudi za nifahamishe kukutana na mume wa dada huyo zinagonga mwamba na mume huyo inadaiwa kuwa ni mfanyabiashara na injini wa mambo ya magari 'Car engineer'


Sakata hilo linaendelea na kwa habari zitakazojili zitaletwa hapahapa

No comments:

Post a Comment