KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 22, 2010

Wanafunzi wawili wagongwa, wananchi wazuia barabara


JANA Eneo la Mtoni Mtongani barabara ya Bagamoyo,Dar es Salaam, kulizuka vurugu kubwa na kugeuka uwanja wa vita kwa takribani masaa nane, baada ya dereva wa daladala kuwagonga wanafunzi wawili wa Shule ya Msingi Tegeta, mmoja kupoteza maisha paoohap

Wanafunzi hao waligongwa majira ya saa 2 asubuhi, wakati wakiwa wakitembea kwa miguuu pembezoni mwa barabaa hiyo.

Taarifa iliyothitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Elias Kalinga, ilisema kuwa dereva huyo mara baada ya kugonga anafunzi hao alikuimbia kwa kuhofia kuuawa na wananchi wenye hasira kali.

Alisema daladala lililogonga wanafunzi hao lilikuwa na namba za usajili T 221 ADF ambapo gari hilo lilishindwa kumudu gari lake baada ya kutaka kujaribu kulipita gari lililokuwa mbele yake.

Alisema wanafunzi hao mmoja alikuwa anasoma darasa la kwanza na mwingine darasa la tatu.

Kufuatia hali hiyo wananchi wenye hasira walitnda barabarani huku wengine walitaka kulichoma moto gari hilo.

Hivyo hali hiyo ilileta mtafaruku mkubwa na ksababisha foleni wananchi wakiweka mawe na wengine kulala barabarani kuzuia magari yasipite barabarani

Kufuatia hali hiyo polisi iliamua fkursha risasi hewa I kutawanya watu hao mahali hapo.

No comments:

Post a Comment