KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Tuesday, July 20, 2010

Wajeruhiwa kwa kuanguka na pikipiki


WATU wawili wamejeruhiwa vibaya baada ya kuanguka na pikipiki majira ya usiku huko maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam.
Watu hao wanaosadikiwa kuwa ni mtu na mpenzi wake walianguka na pikipiki hiyo majira ya saa 5 usiku, na kujeruhiwa vibaya baada ya pikipiki hiyo kuanguka.

Watu hao waliweza kujeruhiwa baada ya dereva huyo ambaye hakufahamika jina lake kushindwa kukata kona kali ya eneo hilo akiwa alikuwa yuko kwenye mwendo kasi.

Hata hivyo mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa chakari kwa kinywaji aliwambia mashuhuda wa tukio hilo kuwa walikuwa wametokea maeneo ya Hongera Bar Sinza kupata kinywaji.

Hata hivyo dada huyo alidai kuwa alimsihi mpenzi wake huyo asinywe kupitiliza kwa kuwa angeshindwa kuendesha pikipiki hiyo.

No comments:

Post a Comment