KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Thursday, July 22, 2010

Waislamu Indonesia Wasali Kuelekea Afrika Badala ya Makka

Waislamu nchini Indonesia wamekuwa wakisali kuelekea Afrika badala ya Makka baada ya kiongozi mmoja wa kidini kujichanga na kuwapotosha watu juu ya uelekeo wa kibla.
Bodi ya waislamu nchini Indonesia ilitoa taarifa jana kwa waislamu nchini humo kuwa ilifanya makosa katika kuwaelekeza watu uelekeo wa kibla.

Kuanzia mwezi machi mwaka huu waislamu nchini humo walikuwa wakisali kuelekea Africa baada ya bodi hiyo kusema kuwa mji mtakatifu wa Makka upo magharibi mwa nchi hiyo.

Waislamu wote duniani wanatakiwa kusali kuelekea kibla kilichopo mjini Makka nchini Saudi Arabia.

Ma'ruf Amin, mwanazuoni wa bodi ya wanazuoni wa Indonesia ULEMA alisema "Baada ya uchunguzi na utafiti wa watalaam imeonekana kuwa watu wamekuwa wakisali kuelekea kusini mwa Somalia na Kenya".

"Sasa tumejua kuwa tunatakiwa tuelekee kaskazini magharibi", alisema.

Mwanazuoni huyo alisema kuwa Waindonesia hawatakiwi kuwa na hofu juu ya kukubalika kwa sala zao kutokana na kuelekea upande tofauti.

"Mungu anajua kuwa binadamu hufanya makosa", alisema mwanazuoni huyo na kuongeza "Allah siku zote husikiliza sala za waja wake".

Indonesia ndio nchi yenye waislamu wengi kuliko nchi zote duniani.

Indonesia ina jumla ya watu milioni 237 asilimia 90 kati yao ni waislamu

No comments:

Post a Comment