KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Amazon MP3 Clips

Thursday, July 22, 2010

Sinema Yasababisha Afanye Mapenzi na Wanaume 1,000


Mwanamke mmoja wa nchini Uingereza ameelezea jinsi alivyovutiwa na tamthilia ya Sex and the City kiasi cha kuamua kufanya mapenzi na wanaume 1,000. Alitimiza lengo lake mwezi uliopita.
Christina Saunders, toka Hertfordshire mashariki mwa Uingereza alifikia lengo lake alilojiwekea miaka 10 iliyopita la kufanya mapenzi na wanaume 1,000 tofauti, limeripoti gazeti la News of the World la Uingereza.

Mambo yote yalianza mwaka 2000 baada ya Christina kuangalia DVD ya tamthilia ya "Sex and the City" ambapo alivutiwa sana na tabia ya mmoja wa wasanii wa tamthilia hiyo Samantha ambaye aliigiza mwanamke anayependa kufanya mapenzi na wanaume tofauti tofauti.

Wakati huo Christina ambaye sasa ana umri wa miaka 30 alikuwa ni mwanafunzi wa chuo kikuu na alikuwa amewahi mara moja tu kufanya mapenzi na mwanaume.

Kwa kuvutiwa na tabia ya msanii huyo, Christina alijiwekea lengo la kufanya mapenzi na wanaume 1,000 tofauti.

Alianza kutongoza wanaume kwenye mabaa na wakati alipokuwa kwenye vakesheni sehemu mbalimbali duniani.

Alikuwa akiweka kumbukumbu na picha kwenye kidaftari chake kila alipomaliza kufanya mapenzi na mwanaume aliyempata.

Alitimiza lengo lake la kutembea na wanaume 1,000 kwa kufanya mapenzi na mwanaume aliyekutana naye kwenye sherehe ya rafiki yake mwezi uliopita.

Christina anakiri kuwa marafiki zake wamegawanyika kuhusiana na tabia yake hiyo, baadhi yao wanampinga na kuona amefanya kitu cha kipuuzi.

"Ninachotaka sasa baada ya kutimiza lengo langu ni kutulia chini, natumaini sijawakasirisha wanaume", alisema Christina.

No comments:

Post a Comment