KARIBU MAISHANI

KARIBU MAISHANI

Monday, July 26, 2010

Wachina kutafuta meli iliyozama miaka 600 nchini Kenya


Kikundi cha wataalam wa mambo ya kale kutoka Uchina wanatarajiwa kuwasili nchini Kenya leo kuanza utafiti wa mabaki ya meli ya kale ya Uchina.

Utafiti huu utatoa mwangaza wa mawasiliano ya kwanza kabisa kati ya Uchina na Afrika Mashariki.

Meli hiyo iliyozama inadhaniwa kufika pwani ya kaskazini ya Kenya karibu na kisiwa cha Lamu mwaka 1418.

Inasadikiwa kwamba Mabaharia kadhaa wa Kichina waliogelea hadi nchi kavu wakati meli yao ilipogonga mwamba na kuzama katika ufukwe wa Lamu.

Uchunguzi wa DNA uliofanyiwa baadhi ya wakaazi wa Siu huko Pate wilayani Lamu umethibitisha kwamba kweli baadhi yao wana asili ya Kichina.

No comments:

Post a Comment